01. Injili inathibitisha kuwa ´Iysaa ni mwanadamu

Soma mwanzo wa Injili Matayo mpaka nambari saba:

“1Ukoo wa Yesu Kristu, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. 2Ibrahimu alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake, 3Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari, Peresi akamzaa Esromu, Esromu akamzaa Aramu, 4Aramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni, 5Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu, Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu, Obedi akamzaa Yese, 6 Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme. Daudi alikuwa baba yake Solmoni ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria, 7Solmoni akamzaa Rehoboamu, Rehoboamu akamzaa Abiya, Abiya akamzaa Asa… “[1]

Imetajwa wazi ya kwamba ´Iysaa ni mja na kwamba Allaah ndiye Mola. Humo imeandikwa vilevile kuwa ´Iysaa amesema:

“Tena imeandikwa: Usimjaribu Mola, Mungu wako.”[2]

Katika mlango huu huu mna ya kwamba Shetani alimnyanyua Masihi na akamchukua kutoka sehemu moja hadi nyingine:

“Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu na akamuweka juu ya kinara cha hekalu 6na akamwambia: “Ikiwa wewe ndiye mwana wa Mungu, basi jitupe chini. Kwa maana imeandikwa: Atawaamrisha Malaika zake na watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.”[3]

Ni vipi Shetani anaweza kumbeba Mwingi wa Rehema? Ametakasika Allaah kutokamana na hayo utakasifu ulio mkubwa!

Kisha Shetani akamuamrisha kumsujudia na kumuabudu na kumvutia kwa mali za kidunia.

“8Halafu Ibilisi akamchukua mpaka kwenye mlima mrefu mno na akamuonyesha milki zote za ulimwenguni na fahari yake 9na akamwambia: “Nitakupa haya yote ukianguka kunisujudia.” 10Ndipo Yesu akamwambia: “Nenda zako, Shetani. Kwa maana imeandikwa: “Msujudie Mola, Mungu wako, umuabudu yeye peke yake.”11”[4]

Vipi Shetani atathubutu kwa Allaah namna hii? Pindi Shetani alitaka ´Iysaa amuabudu alimjibu:

“Nenda zako, Shetani. Kwa maana imeandikwa: “Msujudie Mola, Mungu wako, umuabudu yeye peke yake.”

Tazama namna ambavyo Masihi anajiita mwenyewe “Mwana wa mwanadamu” na wala hakujiita mwana wa Allaah:

“Hakika alikuwa akizunguka katika miji yote ya Israeli kabla ya kuja mwana wa wanadamu.”[5]

Hata hivyo Injili inadai ya kwamba alisikia jinsi anavyoitwa hivyo na hakulikemea.

[1] Matayo 01:01-07

[2] Matayo 04:01-07

[3] Matayo 04:05-06

[4] Matayo 04:05-11

[5] Matayo 10:23

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 11
  • Imechapishwa: 16/10/2016