01. Hadiyth “Yule atakayesoma Suurah al-Kahf siku ya ijumaa… “

736- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesoma Suurah “al-Kahf” siku ya ijumaa, basi Allaah atamwangazia nuru kati ya ijumaa mbili.”[1]

Ameipokea an-Nasaa´iy[2] na al-Bayhaqiy kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pia al-Haakim kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutoka kwa Swahabah. Amesema:

“Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.”

ad-Daarimiy ameipokea katika “al-Musnad” yake kupitia kwa Abu Sa´iyd ambaye amesema:

“Yule atakayesoma Suurah “al-Kahf” usiku wa kuamkia ijumaa, basi Allaah atamwangazia nuru kati yake na kati ya Nyumba ya kale.”

Katika cheni za wapokezi wote, isipokuwa tu al-Haakim, yuko Abu Haashim Yahyaa bin Diynaar ar-Rumaaniy. Wengi wanaona kuwa ni mwaminifu. Cheni zengine zote za wapokezi ni aminifu.

[1] Swahiyh.

[2] Maneno ya mtunzi wa kitabu yanaweza kufahamika kwamba an-Nasaa´iy hakuipokea isipokuwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Lakini ameipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutoka kwa Swahabah, kama alivofanya al-Haakim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/455)
  • Imechapishwa: 08/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy