01. Hadiyth “Hakuna mja yeyote muislamu anayeswali… “

579- Umm Habiybah Ramlah bint Abiy Sufyaan (Radhiya Allaahu ´anhumaaa) amesimulia kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakuna mja yeyote muislamu anayeswali kila siku kwa ajili ya Allaah Rak´ah kumi na mbili ambazo ni za kujitolea – na sio zile za faradhi[1] – isipokuwa Allaah (Ta´ala) atamjengea nyumba Peponi au atajengea nyumba Peponi.”[2]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na at-Tirmidhiy ambaye amezidisha:

“Rak´ah nne kabla ya Dhuhr, mbili baada yake, mbili baada ya Maghrib, mbili baada ya ´Ishaa na mbili kabla ya swalah ya Fajr.”

[1] Hapa ni kwa minajili ya kutilia mkazo na kuondosha ile sintofahamu. Namna hii inatakiwa kufanya wakati kunapohitajia kufanya hivo.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/455)
  • Imechapishwa: 08/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy