216 – Abu Ayyuub al-Aswaariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uzuri uliyoje wa wale wanaosugua (المتخللون)[1] katika ummah wangu… “[2]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” na Imaam Ahmad, wote wawili kwa kifupi kutoka kwa Abu Ayyuub na ´Atwaa´.

217 – at-Twabaraaniy pia ameipokea katika “al-Mu´jam al-Awsatw” kupitia kwa Anas. Njia zake zote zinazungukia kwa Waaswil bin ´Abdir-Rahmaan ar-Ruqaashiy ambaye ni mwenye kuaminika kwa mujibu wa Shu´bah na wengineo[3].

[1] Imekuja katika “an-Nihaayah”:

“Kusugua ni kupitisha vidole kwenye meno ili kuondosha yale mabaki ya chakula yaliyoko kati ya meno na kusugua ndevu na kati ya vidole vya mikononi na miguuni wakati wa kutawadha.”

[2] Nzuri kupitia zingine.

[3] Waaswil bin ´Abdir-Rahmaan ar-Ruqaashiy hakutajwa kabisa katika Hadiyth hii. Aliyetajwa ni Waaswil bin as-Saa-ib ar-Ruqaashiy – na ambaye ni dhaifu kwa makubaliano. Isitoshe anakosa katika cheni ya wapokezi ya Anas, ambayo ni yenye nzuri yenye kuitia nguvu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/205)
  • Imechapishwa: 16/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy