01. Hadiyth “Hakuna yeyote katika nyinyi atakayeeneza vizuri wudhuu´ kisha akasema… “

224 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna yeyote katika nyinyi atakayeeneza vizuri wudhuu´ kisha akasema:

أشهدُ أن لا إلهَ إلَّا اللهُ وأشهدُ أنَّ محمَّدًا عبدُه ورَسولُه

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”

isipokuwa atafunguliwa milango ya minane ya Pepo. Ataingia kupitia mlango wowote anaotaka.”[1]

Ameipokea Muslim. Imekuja kwa Abu Daawuud na Ibn Maajah:

فيحسن الوضوء

“Hakuna yeyote katika nyinyi atakayetia vizuri wudhuu´… “[2]

at-Tirmidhiy pia ameipokea kwa ziada isemayo:

اللَّهمَّ اجعَلْني مِن التَّوَّابِينَ، واجعَلْني مِن المُتطهِّرِينَ

“Ee Allaah! Nifanye kuwa miongoni mwa wenye kutubu na nifanye kuwa miongoni mwa wenye kujitwahirisha.”

Hata hivyo imetiwa kasoro.

[1] Swahiyh.

[2] Abu Daawuud amezidisha kwa kusema:

“Kisha akanyanyua macho yake mbinguni na kusema…

Katika cheni ya wapoekezi kuna mtu ambaye hakutajwa jina, ikiwa na maana ni ziada dhaifu na inapingana na zilizo Swahiyh – kwa hivyo haikusihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/208-209)
  • Imechapishwa: 23/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy