331 – Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن أكلَ من هذه الشجرةِ (يعني الثومَ) فلا يقرَبَنَّ مسجدَن

 “Anayekula kutoka katika mti huu – yaani kitunguu saumu – basi asiukurubie msikiti wetu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Imekuja kwa Muslim:

فلا يَقْرَبَنَّ مساجدَنا

“… asikurubie misikiti yetu.”

Imekuja kwa Abu Daawuud:

مَن أكل من هذه الشجرةِ فلا يقرَبَنَّ المساجد

“Anayekula kutoka katika mti huu basi asikurubie misikiti.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/254)
  • Imechapishwa: 08/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy