00. Misingi ya imani na misingi ya ´Aqiydah inayompambanua muumini na kafiri

Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu, ambaye anamuwafikisha amtakaye katika waja Wake kutokana na neema na fadhilah Zake. Aidha anamkosesha nusura amtakaye ambapo akatumbukia ndani ya ukafiri kutokana na hekima na uadilifu Wake – swalah, amani na baraka zimwendee mja na Mtume Wake; Mtume wetu Muhammad ambaye ndiye mwisho wa Manabii na Mitume Yake. Kupitia yeye Allaah amemukoa amtakaye kwa kumtoa kwenye ukafiri na upotofu na kumwingiza katika imani, nuru na mwangaza wake. Vilevile swalah na amani zimwendee kizazi chake, Maswahabah na wafuasi wake.

Ama baada ya hayo;

Katika ”as-Swahiyh” ya Muslim na kwenginepo imethibiti kupitia Hadiyth ya ´Umar bin al-Khattwaab ya kwamba Jibriyl (´alayhis-Salaam) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika umbile la mtu ambapo akamuuliza kuhusu Uislamu, imani, ihsaan, Saa na alama zake ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamjibu kuhusu imani:

”Ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar kheri na shari yake.”[1]

Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anabainisha ndani ya Hadiyth hii tukufu misingi ya imani na misingi ya ´Aqiydah ambayo anapambanuka kwayo muumini kutokana na kafiri. Nayo ni misingi sita:

[1] Muslim (08) na tamko ni lake na al-Bukhaariy (50) pamoja na kutofautiana kwa baadhi ya matamshi yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 05-06
  • Imechapishwa: 19/03/2023