Swali: Zakaat-ul-Fitwr inawawajibikia watu gani?

Jibu: Inamuwajibikia kila muislamu mvulana kwa msichana, mdogo kwa mkubwa, sawa mtu awe amefunga au hakufunga. Kama kwa mfano mtu alikuwa msafiri na hakufunga lakini hata hivyo Zakaat-ul-Fitwr inamlazimu.

Kuhusu ambaye imependekezwa kwake wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa imependekezwa kukitolea kipomoko kilichomo tumboni na wala sio wajibu.

Kuizuia ni jambo la haramu kwa kuwa ni kunapingana na yale yaliyofaradhisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ilivyotangulia punde tu katika Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifaradhisha Zakaat-ul-Fitwr kuwa pishi ya tende au pishi ya shayiri kwa kumaliza Ramadhaan.”

Ni jambo linalojulikana kwamba kuacha kilichofaradhishwa ni haramu na mtu anapata dhambi na maasi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/259)
  • Imechapishwa: 21/06/2017