Swali: Je, inafaa kuwapa zakaah mizunguko ya kielimu inayosomesha Qur-aan?

Jibu: Hapana. Zakaah haitolewi kwa ajili ya kuhifadhi Qur-aan. Hawa wanapewa swadaqah na michango mingine. Wasipewi zakaah. Zakaah ni kwa ajili ya mafukara, masikini na aina nyenginezo zilizowekwa katika Shari´ah. Kuhusu nyanja zengine za mambo ya kheri wanapewa swadaqah na michango mingine. Miongoni mwa mataasisi hayo ni zile zinazojenga misikiti, masomo na kusomesha Qur-aan. Mataasisi kama haya hayapewi zakaah. Zakaah wanapewa wale watu aina saba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 23/04/2021