Swali: Sisi ni kikosi cha ndugu ambao tuko na ardhi ambayo tunaitafutia soko sasa kwa miaka nane. Ardhi hiyo tumeiuza mwaka uliopita. Je, ni lazima kuitolea zakaah ardhi hiyo kwa ile miaka iliopita?

Jibu: Ndio, kila mwaka. Muda wa kuwa inatafutiwa soko, basi kila inapotimiza mwaka inatakiwa kukadiriwa thamani yake na kutolewa zakaah.

Swali: Kila mmoja katika sisi anatakiwa kutoa fungu lake la zakaah au itolewe kwa pamoja?

Jibu: Mtaamua nyinyi. Mnaweza kuitoa kwa pamoja au kila mmoja kivyake. Muhimu itoleeni zakaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 23/04/2021