33. Vipi swawm ya anayeeneza umbea na kusengenya?

Swali 33: Je, kusengenya na kueneza uvumi kunamfunguza mfungaji mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Kusengenya na kueneza uvumi havifunguzi. Lakini hata hivyo vinapunguza swawm. Allaah (Ta´ala) amesema:

يأيها الذينءامنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم لعلكم تتقون

 “Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule asiyeacha maneno ya uongo, kuyatendea kazi na ujinga, basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”

[1] 02:183

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 30
  • Imechapishwa: 23/04/2021