Swali: Je, magari ya kibinafsi yanatolewa zakaah?

Jibu: Hapana. Hakuna zakaah juu ya kila kitu ambacho mtu hukitumia mwenyewe. Isipokuwa tu mapambo ya dhahabu na fedha. Vinginevyo vitu binafsi havitolewi zakaah; ni mamoja ni gari, ngamia na mashine ya kilimo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Muislamu halazimiki kumtolea zakaah mtumwa wala farasi wake.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1464) na Muslim (982).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/210)
  • Imechapishwa: 08/05/2021