Swali: Mabarabarani na kwenye taa za trafiki wako watu wanaokuja na kuomba zakaah. Je, inafaa kwangu kuwapa zakaah au ni lazima kwanza kuhakikisha kama kweli ni wahitaji?

Jibu: Ikiwa hujui kuwa ni matapeli na waongo, basi unatakiwa kuwapa. Unatakiwa kuzingatia ile hali yao ya nje:

وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ

“Katika mali zao kuna haki maalum; kwa mwenye kuomba na asiyeomba.”[1]

Huyu ni mwombaji. Ikiwa hujui kuwa ni mwongo, basi unatakiwa kuwapa. Itakiwa katika dhimma yao.

[1] 51:19

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 27/04/2021