Wanaoitwa Muhammad hawatoadhibiwa?


Swali: Je, kuna Hadiyth Swahiyh yenye manaa inayosema kuwa kila ambaye jina lake ni Muhammad hatoadhibiwa kwa ajili ya heshima ya jina hili na mwenye nalo?

Jibu: Huu ni ukhurafi. Jina halisaidii kitu. Kinachoangaliwa ni matendo na ufuataji. Hili ni kama mfano wa maneno ya al-Buuswayriy:

Mimi nina dhimma kwake kwa kuitwa Muhammad

Yeye ndiye kiumbe pekee awezae kunitimizia dhimma yangu

Huu ni ukhurafi na batili. Jina halitoshelezi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (46) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2152
  • Imechapishwa: 06/09/2020