al-Fawzaan kuhusu sujuud za cacheza boli


Swali: Ni kweli kuwa umefutu kwamba yale yanayofanywa na baadhi ya wachezaji mpira wanaposujudu kwa ajili ya furaha ya kushinda na mfano wa hayo inachukuliwa ni Bid´ah pamoja na hivyo inazingatiwa ni katika Sujuud-ush-Shukr?

Jibu: Sujuud-ush-Shukr haikuwekwa isipokuwa pale ambapo mtu anapata neema mpya au anaondokewa na tatizo. Kushinda kwa mpira sio neema. Hii ni neema kwa waislamu? Waislamu wamefaidika nini nao? Bali yeye mwenyewe huyo mchezaji amefaidika nini? Huku sio kupata neema mpya. Kwa hivyo kusujudu inakuwa Bid´ah kwa sababu ni kitendo kisichokuwa na sababu yoyote ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (46) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2152
  • Imechapishwa: 06/09/2020