Wanalala na kupitwa na swalah kwa hoja eti wamepewa udhuru

Swali 23: Wako baadhi ya watu ambao wanalala na kuacha swalah kwa kukusudia na wanatumia hoja maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka… ”[1]

Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Hadiyth inamkusudia yule ambaye hakuzembea. Kuhusu mtu ambaye anafanya uzembe haweki alamu wala haiambii familia yake kumuamsha anapata dhambi. Kwa sababu amezembea kutekeleza kitu ambacho Allaah amemuwajibishia.

[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 36
  • Imechapishwa: 24/10/2018