Mashaytwaan wana sikukuu nne kwa mwaka mbali na sikukuu zengine. Miongoni mwa sikukuu hizo kunaingia vilevile sikukuu ya pindi mchana unapokuwa mrefu na mfupi zaidi kwa mwaka. Kuhusu sikukuu yao kubwa ni ile ambayo inaitwa Halloween. Hii ni sikukuu ya tangu hapo kale ambayo waadhimishaji walikuwa wakisherehekea kwa kufanya sikukuu kubwa kabisa wakimfanyia mungu wao wa Mauti. Hayo yalitokea takriban miaka 200 ya nyuma.

Walikuwa wakiamini kuwa mungu huyu huziachia roho zilizokufa katika usiku huo na kurejea katika zile nyumba ambazo walikuwa wakiishi hapo kaba. Haya yanatendeka kabla ya kuingia mwaka mpya.

Kuhusu roho ovu, ni zenye kufungwa gerezani katika viwiliwili vya wanyama kwa muda wa miezi kumi na mbili. Katika usiku wa Halloween zinaachwa, kama roho zengine, ili zirejee katika nyumba zao za zamani.

Wanaona kuwa ni wajibu kwa wale wakazi wa nyumba hizo kuwawekea chakula katika usiku huo. Chakula hicho anatengenezewa mungu huyu wa Mauti ili azisamehe roho hizo ovu ili zisirejee kama wanyama. Ikiwa sherehe hiyo haikufanywa, basi roho hiyo itaroga na kuilaani nyumba hiyo.

Watu hao walikuwa wanachukulia Halloween kuwa ndio siku bora katika masiku ya mwaka, kwa sababu ndio inakuwa wepesi zaidi kuwasiliana na roho ambayo inazunguka ulimwenguni baada ya mungu wao kuziacha huru.Mashaytwaan wana sikukuu nne kwa mwaka mbali na sikukuu zengine. Miongoni mwa sikukuu hizo kunaingia vilevile sikukuu ya pindi mchana unapokuwa mrefu na mfupi zaidi kwa mwaka. Kuhusu sikukuu yao kubwa ni ile ambayo inaitwa Halloween. Hii ni sikukuu ya tangu hapo kale ambayo waadhimishaji walikuwa wakisherehekea kwa kufanya sikukuu kubwa kabisa wakimfanyia mungu wao wa Mauti. Hayo yalitokea takriban miaka 200 ya nyuma.

Walikuwa wakiamini kuwa mungu huyu huziachia roho zilizokufa katika usiku huo na kurejea katika zile nyumba ambazo walikuwa wakiishi hapo kaba. Haya yanatendeka kabla ya kuingia mwaka mpya. Kuhusu roho ovu, ni zenye kufungwa gerezani katika viwiliwili vya wanyama kwa muda wa miezi kumi na mbili. Katika usiku wa Halloween zinaachwa, kama roho zengine, ili zirejee katika nyumba zao za zamani. Wanaona kuwa ni wajibu kwa wale wakazi wa nyumba hizo kuwawekea chakula katika usiku huo. Chakula hicho anatengenezewa mungu huyu wa Mauti ili azisamehe roho hizo ovu ili zisirejee kama wanyama. Ikiwa sherehe hiyo haikufanywa, basi roho hiyo itaroga na kuilaani nyumba hiyo.

Watu hao walikuwa wanachukulia Halloween kuwa ndio siku bora katika masiku ya mwaka, kwa sababu ndio inakuwa wepesi zaidi kuwasiliana na roho ambayo inazunguka ulimwenguni baada ya mungu wao kuziacha huru.

  • Mhusika: Yuusuf bin Ahmad al-Bin´aliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ubbaad-ush-Shaytwaan, uk. 95-96
  • Imechapishwa: 24/10/2018