“Waacheni watu waamini wanachokitaka”  

Swali: Baadhi ya watu wanasema “waacheni watu waamini yale wanayotaka, Uislamu umempa mtu khiyari ya kuamini”.

Jibu: Huu ni uongo. Uislamu haukubaliani na imani za kikafiri. Unazipinga na kuwapiga vita wenye nazo mpaka waamini. Huu ndio Uislamu. Ni kwa nini Jihaad katika njia ya Allaah imewekwa? Si jingine isipokuwa ni kwa sababu ya kutokomeza mbali shirki na kuinusuru Tawhiyd na dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Uislamu haukubaliani na imani batili. Kinyume chake unazipinga na kuwapiga vita wenye nazo pale watapolingania kwazo na kuendelea juu yazo na kuzitetea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-18.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020