Swali: Je, ni kafiri mtu anayemsujudia asiyekuwa Allaah, anachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah na anaweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah na anashuhudia ya kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah?

Jibu: Bila ya shaka yoyote. Ikiwa anakusudia mambo haya na anajua kuwa kuchinja ni ´ibaadah na kumsujudia asiyekuwa Allaah vilevile ni ´ibaadah na akamfanyia haya asiyekuwa Allaah, hakuna shaka yoyote juu ya ukafiri wa huyu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-18.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020