al-Fawzaan kumhukumu kafiri kwa dhati yake Moto baada ya kufa kwake

Swali: Myahudi au mnaswara akifa ahukumiwe kwa dhati yake kwamba ni mtu wa Motoni?

Jibu: Allaah hakukukalifisha kwa hili. Hujui ghaibu. Pengine alitubia kabla ya kufa kwake. Usihukumu mtu kwa dhati yake ya kwamba ni mtu wa Motoni au wa Peponi isipokuwa kwa dalili kutoka katika Qur-aan au Sunnah. Tunaratajia Pepo kwa mtenda mazuri na tunakhofia Moto kwa watenda maovu. Hatumkatii yeyote hukumu ya Pepo wala Moto isipokuwa yule aliyeshuhudiliwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah hakukukalifisha jambo hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-18.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020