Vipi mwanamke atachagua mume bora?


Swali: Ndugu yangu anataka kuoa binti, lakini mama yake anakataa kwa kuwa ana ndevu. Vipi anaweza kumkinaisha?

Jibu: Amuwekee wapatanishaji wazuri katika Waislamu mpaka wamweleweshe Kishari´ah ni nani anayestahiki kumuoa binti yake ikiwa kweli anampenda binti yake na hii ni katika tabia ya binaadamu kumpendea mtoto wake kheri, sawa ni wakiume au wakike. Kwa makubaliano haya ya watu wenye hekima na watoaji nasaha wazuri, atakinaika [mamake mwanamke] kuolewa na kijana huyu, mwenye ndevu, mwenye kuswali, mpwekeshaji [mtu wa Tawhiyd]. Asishtuke sana na ndevu, bali aipe kipaumbele kwanza Tawhiyd, na awe mwenye kutekeleza Shari´ah zote kama Swalah, tabia nzuri. Na katika Hadiyth:

“Atapokujieni mnayemridhia dini yake na tabia yake, basi muozesheni. Msipofanya hivyo itakuwa fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.”

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Imechapishwa: 19/09/2020