Vipi kupata radhi za wazazi baada ya kukosana nao?

Swali: Mimi nilikuwa ni mwenye kuwakosea wazazi wangu katika haki nyingi na baba yangu aliomba du´aa dhidi yangu. Unaninasihi kuwafanyia nini katika kuwatendea wema?

Jibu: Kwanza mlango wa tawbah uko wazi. Ni juu yako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

Pili ikiwa wazazi wako bado wako hai au mmoja wao yuko hai, ni juu yako kumuomba radhi ili wakusamehe kwa yale uliyofanya.

Tatu baada ya hapo ni juu yako kuwatendea wema. Ikiwa wote wameshakufa, au mmoja wao ameshakufa, ni juu yako kuwaombea du´aa, msamaha, uwatolee swadaqah kwa wingi na ikiwa wana madeni uwalipie nayo. Huku ni kuwatendea wema baada ya kufa kwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2105
  • Imechapishwa: 30/06/2020