Anayekusanya sifa za unafiki wa kimatendo

Swali: Sifa za mnafiki tatu zikikusanyika kwa mtu zinampelekea katika unafiki mkubwa? Ni ipi maana ya Hadiyth inayosema kuwa hazikusanyiki kwa mtu isipokuwa anakuwa mnafiki safi kabisa?

Jibu: Haina maana kuwa anakuwa ni mnafiki mwenye unafiki mkubwa. Maana yake ni kwamba anakuwa ni mnafiki mwenye unafiki wa kimatendo na hali yake inakuwa khatari zaidi. Kwa sababu unafiki wa kimatendo unatofautiana pia. Kuna unafiki wa kimatendo mwepesi na mwingine khatari zaidi. Ukiwa mkubwa kwa mtu huenda ukampelekea katika unafiki mkubwa. Hakuna kheri yoyote katika unafiki sawa mkubwa au mdogo. Mtu asichukulie usahali kwa unafiki. Ukisikia kuwa kitendo fulani katika unafiki mdogo usiuchukulie usahali kwa sababu kwanza ni unafiki na pili unaweza kumpelekea mtu katika unafiki mkubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2105
  • Imechapishwa: 30/06/2020