Utasamehewa lini kama hukusamehewa mwezi huu?

Huu ndio mwezi wa msamaha. Atasamehewa lini yule ambaye hakusamehewa Ramadhaan? Ni hasara kubwa. Lakini mwenye furaha ni yile aliyewafikishwa na Allaah na akajirekebisha. Himdi zote zinamstahikia Allaah kuona milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya Moto hufungwa na shaytwaan hufungwa. Kila usiku kunasemwa:

“Ee mwenye kutaka kheri fika! Ee mwenye kutaka shari koma! Kuna watu Allaah huwaachia huru na Moto. Hilo linakuwa kila usiku.”

Hizi ni fadhila kubwa. Tunamuomba Allaah atutunukie nazo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ramadhan%201-9-1436.mp3
  • Imechapishwa: 19/05/2020