Swali: Inajuzu kufuga makucha kwa ajili ya mapambo?

Jibu: Hapana. Mambo matano ni katika maumbile moja wapo ni kukata kucha. Haifai kwake kuyaacha yakakuwa marefu. Ni katika sifa ya wanyama. Akate makucha yake kila wiki au kwa kulingana, masharubu yake na aondoshe nywele za kwapani na za sehemu za siri. Asiziache zikakuwa. Ni katika maumbile, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuziacha zikakuwa ni katika kujifananisha na makafiri na wapotevu. Kuna watu wanaoitwa “hippies”. Hawakati si nywele wala kucha zao. Wako kama wanyama. Uchafu na taka imewaambata. Wamekuwa wamabaya. Unataka kujifananisha na hippies?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir%20ayat-03-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020