Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mwanamke na huku amefunua mikono yake?

Jibu: Swalah yake si sahihi. Mwili mzima wa mwanamke hautakiwi kuonekana katika swalah isipokuwa uso wake ikiwa mbele yake hakuna wanaume ambao sio Mahram. Hatakiwi kuonyesha kitu katika mwili wake wakati wa swalah. Akifanya hivo swalah yake inabatilika. Kufunika ´Awrah ni miongoni mwa masharti ya kusihi kwa swalah – mwili wote wa mwanamke ni katika swalah ni ´Awrah isipokuwa uso wake midhali mbele yake hakuna wanaume ambao si Mahram zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir%20ayat-03-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020