Unasihi wudhuu´ wa ambaye anaanza upande wa kushoto kabla ya wa kuume?

Swali 03: Unasihi wudhuu´ wa ambaye anaanza upande wa kushoto kabla ya wa kuume[1]?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana katika jambo hilo. Lililo salama zaidi ni yeye atoke kwenye tofauti na arudi kutawadha upya ikiwa alianza upande wa kushoto kabla ya upande wa kulia wakati wa kuosha kwa mfano mikono au miguu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkitawadha basi anzeni na kuume kwenu.”

Isitoshe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akianza kwa upande wa kulia. Lengo ni ili wudhuu´ wake usalamike kutokakamana na tofauti.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuna-athar-sahihi-ya-aliy-kwamba-alianza-upande-wa-kushoto-wakati-wa-kutawadha/ 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 32
  • Imechapishwa: 31/07/2018