Umandemande kwenye chupi baada ya kuamka

Swali: Wakati fulani pindi ninapoamka kutoka usingizini ninaona maji maji kwenye chupi. Sijui kama ni manii au madhiy…

Jibu: Ni manii. Umemwaga pasi na kujua. Ukiona athari ya manii bila ya kujua, ni lazima uoge. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maji yanatokamana na maji.”

Bi maana mtu anatakiwa kuoga baada ya kumwaga pasi na kujali ukihisi hilo au usihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020