Ulaghai wa bili


Swali: Tunafanya kazi ya kukodisha vifaa. Baada ya kumalizika kwa kazi anaomba wakala kuandika kiwango cha juu zaidi katika bili kuliko uhalisia. Kwa mfano makubaliano ni pesa 500 basi anaomba kuandika pesa 600 katika bili…

Jibu: Hili halijuzu. Ni haramu. Huu ni uongo na ulaghai na haijuzu. Usiandike isipokuwa uhalisia wa mambo, sawa na biashara yenyewe, na usizidishe kitu ukaja kudhulumu kampuni na mfanya kazi. Andika kama mambo yalivyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (84) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17577
  • Imechapishwa: 13/02/2021