Anataka kumuoa msichana wa mjomba ambaye walinyonya ziwa moja

Swali: Msichana wa mjomba wangu akinyonya pamoja nami kutoka kwa mama yangu na wakashuhudia jambo hilo zaidi ya mtu mmoja – je, anakuwa dada yangu na ndugu zangu wengine waliobaki? Je, inakuwa ni haramu kwa ndugu zake wa kiume wa mwanamke huyo kuwaoa dada zangu?

Jibu: Ikithibiti kuwa msichana huyo alinyonya mara tano ndani ya ile miaka miwili ya kwanza kwa ushahidi wa waadilifu, basi anakuwa ni binti ya mwanamke huyu ambaye kanyonya kutoka kwake. Pia watoto wake wote wa kiume na wa kike wanakuwa ni ndugu wa msichana huyu ambaye alimnyonyesha. Kuhusu ndugu zake wa damu kama vile baba yake na mama yake wa koo hawana mafungamano yoyote ya unyonyeshaji huu. Unyonyaji unahusiana na yule mnyonyweshwaji peke yake na watoto wake na pia unahusiana na yule mwanamke mnyonyeshaji peke yake, mume wake na ndugu jamaa zake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 13/02/2021