Ufafanuzi wa maneno ya Imaam Ahmad kuhusu Basmalah wakati wa wudhuu´

Swali: Kuhusu masuala ya Basmalah wakati wa wudhuu´ Imaam Ahmad amesema “Hakukuthibiti juu ya hilo kitu”. Je, hii ina maana ya kwamba ni sahihi kutawadha bila ya kusema “Bismi Allaah”?

Jibu: Kwa mujibu wa Imaam Ahmad, Basmalah ni wajibu miongoni mwa mambo ya wajibu ya wudhuu´. Kwa kauli yake:

“Hana wudhuu´ yule ambaye hakutaja Jina la Allaah juu yake.”

Kauli ya Imaam Ahmad “Hakukuthibiti juu ya hilo kitu”, yaani hakuna mapokezi sahihi juu ya hilo. Lakini kumepokelewa Hadiyth nyingi dhaifu ambazo zinapeana nguvu. Imaam Ahmad hakusema “Hakukupokelewa juu ya hilo kitu”, bali amesema “Hakukuthibiti”, bi maana hakukusihi juu yake kitu. Hadiyth dhaifu zikiwa nyingi zinapeana nguvu. Kwa ajili hiyo ndio maana Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameonelea kuwa ni wajibu kuleta Tasmiyah wakati mtu atapokumbuka. Ama akisahau, wudhuu´ wake ni sahihi.

Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa kusema “Bismillaah” kabla ya kuanza kutawadha ni Sunnah na sio wajibu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (69) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13888
  • Imechapishwa: 16/11/2014