Wanawake kwenda katika michezo na minasaba ya masherehe

Swali: Ni ipi hukumu ya wanawake kuhudhuria sehemu za michezo ikiwa ni kama wanavyodai ni kwa vigezo vya Kishari´ah, bi maana watawekewa sehemu yao maalum…

Jibu: Vigezo vya Kishari´ah ni yeye kubaki nyumbani kwake na asiende sehemu za michezo wala kwenye masherehe. Hivi ndivyo vidhibiti vya Kishari´ah. Akitoka kwenda kwenye michezo, basi ametoka nje ya vidhibiti vya Kishari´ah. Hata kutoka kwenda misikiti Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah na majumba yao ni bora kwao.”

Hii ni misikiti ambapo ni sehemu za ´ibaadah. Tusemeje sehemu za michezo na sehemu za masherehe? Khaswa kama jinsi mnavyojua yanayotokea sehemu za michezo na masharehe miongoni mwa mambo maovu na mchanganyiko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (69) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13888
  • Imechapishwa: 16/11/2014