Takbiyr katika masiku ya kuchinja ni kila wakati

Swali: Takbiyr katika yale masiku ya kuchinja inakuwa baada ya swalah pekee au ni kila wakati?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba Takbiyr katika yale masiku ya kuchinja imependekezwa kuileta kila wakati. Allaah (Ta´ala) ameelekeza hilo katika Qur-aan katika Kitabu kitukufu:

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ

“Mdhukuruni Allaah katika zile siku zinazohesabika.”[1]

[1] 02:203

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1676
  • Imechapishwa: 25/09/2020