Ni ipi hukumu ya anayeswali peke yake nyuma ya safu?

Swali: Akija mwanamme na swalah ya mkusanyiko inaswaliwa na safu imekamilika – aswali nyuma ya safu au afanye nini?

Jibu: Mtu akija na safu imekamilika basi asubiri na asifanye haraka. Asogelee safu pengine akapata upenyo. Ajitahidi huenda akapata upenyo au asimame upande wa kulia kwa imamu ikiwa kuna nafasi. Asiswali peke yake. Wapo wanachuoni waliosema kuwa aswali peke yake kutokana na dharurah. Lakini hata hivyo maoni ya sawa ni kwamba asiswali peke yake. Bali anachotakiwa ni kusubiri mpaka atakapopata upenyo katika safu au ajitokeze mmoja aswali pamoja naye. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna swalah kwa mwenye kuswali peke yake nyuma ya safu.”

Vilevile wakati alipomaliza kuswali akamuona bwana mmoja ameswali peke yake ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha airudi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4616/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%86%D9%81%D8%B1%D8%AF-%D8%AE%D9%84%D9%81-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%81
  • Imechapishwa: 25/09/2020