Swali: Mwenye kuingia msikitini na muadhini anaadhini amfuate muadhini au aswali moja kwa moja Tahiyyat-ul-Masjid?

Jibu: Ikiwa anahitaji kukaa baada tu ya adhaana ili aweze kusikiliza mawaidha au darsa aswali Sunnah hiyo na huku muadhini anaadhini. Hakuna neno kwa sababu aweze kupata nafasi baada ya adhaana kwa ajili ya kusikiliza darsa au mfano wa hayo. Ikiwa sio kwa lengo hilo anachotakiwa ni kumfuata muadhini. Pindi atapomaliza ndipo aswali Tahiyyat-ul-Masjid.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/27-06-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 16/07/2017