Anataka kutumia dawa ya kuleta maziwa kifuani kwa lengo la kumnyonyesha mtoto asiyekuwa wake

Swali: Kuna mwanamke anasema kuwa anataka kumlea mtoto wa kiume mdogo aliye na miezi sita. Anauliza kama inafaa kutumia sindano au dawa kwa ajili ya kuleta maziwa na kumnyonyesha mtoto huyu ili awe Mahram wake katika mustaqbal?

Jibu: Hapana. Haijuzu kufanya hivo. Akiwa na maziwa na mtoto akawa anahitajia kwa sababu hajaanza kula chakula. Katika hali hii amfanyie wema na amnyonyeshe. Anakuwa Mahram wake akifikisha kiwango cha unyonyeshaji. Ama ikiwa ni uonyonyeshaji wa hila haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/27-06-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 16/07/2017