Swali: Kuna ndugu mmoja amenieleza kuwa baada ya Allaah amemshtakia tatizo lake mwanachuoni mmoja miongoni mwa wanachuoni wakubwa lililomfika yeye na watoto wake. Shaykh huyu akamwambia asome Suurat-ul-Anbiyaa´ wakati wa kulala kwa muda wa siku sabini kisha utamuona aliyekufanyia kijicho katika siku ile ya mwisho usingizini mwako. Je, afanyie kazi fatwa hii?

Jibu: Sijui kuwa ina msingi. Sijui dalili yoyote kuhusu hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-29.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020