Sujuud ya kusahau wakati wa kuacha jambo la wajibu katika swalah

Swali: Je, maamuma ni lazima alete Sujuud-us-Sahuw akiacha jambo la wajibu au jambo lililopendekezwa?

Jibu: Sujuud-us-Sahuw kwa kuacha jambo lililopendekezwa sio wajibu, katika hali hii imependekezwa. Lakini ikiwa mtu ameacha jambo la wajibu basi ni wajibu alete Sujuud-us-Sahuw.

Hata hivyo ikiwa atakuwa na Imamu kuanzia mwanzo wa Swalah kisha maamuma akapitikiwa na kusahau – na si Imamu – kwa kuacha jambo la wajibu, hili linabeba Imamu na yeye hana juu yake Sujuud-us-Sahuw. Lakini ikiwa ni mwenye kutanguliwa na akapitikiwa na kusahau katika yale ambayo aliswali peke yake baada ya Imamu, anatakiwa kusujudu kwa kusahau kwake. Hata kama atasahau pamoja na Imamu wake na yeye ni mwenye kutanguliwa kwa Rakaa moja au zaidi, anatakiwa kuleta Sujuud-us-Sahuw kwa yale aliyosahau pamoja na Imamu wake ikiwa ni mwenye kutanguliwa na vilevile asujudu kwa yale aliyoswali peke yake mbali na Imamu wakati ataposimama baada ya kutoa Salaam.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-8-5.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014