Sujuud ya kusahau kwa aliyesahau kusoma Suurah baada ya al-Faatihah

Swali: Ni ipi hukumu lau imamu atasahau katika swalah za kusoma kwa sauti kusoma Suurah baada ya Faatihah?

Jibu: Ni Sunnah. Ikiwa amesahau kusoma baada ya Faatihah kitu katika Qur-aan katika zile Rak´ah mbili za mwanzo, huyu ameacha Sunnah. Inapendekeza kwake kuleta Suujud ya kusahau kwa minajili ya mapendekezo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-8-5.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014