Kuleta “Takbiyr” Wakati Wa Kwenda Na Kuinuka Katika Sujuud-us-Sahuw

Swali: Imamu akiswali Rakaa tano katika Swalah ya Dhuhr na akatoa Salaam na baada ya muda mfupi akakumbuka kuwa hakuleta Sujuud-us-Sahuw. Je, aseme “Allaahu Akbar” au hapana?

Jibu: Aseme “Allaahu Akbar” kwa ajili ya Sujuud na aseme “Allaahu Akbar” kwa ajili ya kuinuka. Atapoenda katika Sujuud aseme “Allaahu Akbar” na atapoinuka kusoka kwenye Sujuud aseme “Allaahu Akbar” kama ilivo Sujuud ya Swalah. Ni vile vile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-8-5.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014