Siku mbili zimezidi juu ya ada alozowea kupata

Swali: Mwanamke amezowea kupata hedhi yake siku saba mwanzoni mwa mwezi. Hedhi ikamjia kwa siku zake lakini hata hivyo kukazidi siku mbili na damu imebadilika na haina sifa ya hedhi. Lipi linalomlazimu?

Jibu: Maadamu haikukatika ni hedhi. Siku zinaweza kuzidi. Siku za hedhi zinaweza kuzidi midhali haikukatika bali imekamatana na hedhi, ni hedhi hata kama itakuwa damu kidogo. Hata damu ya rangi ya zanbarau [uchafu] na umanjano ikikamatana na hedhi na isikatike bado anahesabika kuwa yuko na hedhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (32) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-16.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020