Shiy´ah al-Jazaairiy akithibitisha kwamba elimu ya maimamu ni bora kuliko ya Mitume

Tano: Khabari zilizohifadhiwa ni kwamba: elimu ya maimamu ni kamilifu zaidi kuliko elimu ya kila Mtume. Hilo ni kwa sababu miongoni mwa jumla zake wana elimu ya lile jina likubwa ambalo lina herufi sabini na tatu. Herufi moja Allaah (Subhaabah) ameificha Kwake Mwenyewe. Herufi zengine sabini na mbili alimfunza nayo Mtume na akamwamrisha awafunze nayo watu wa Nyumbani kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu Mitume wengine waliobaki (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam), as-Swaadiq amesema: “´Iysaa (´alayhis-Salaam) alipewa herufi mbili ambazo alikuwa akizitendea kazi, Muusa (´alayhis-Salaam) alipewa herufi nne, Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alipewa herufi nane, Nuuh (´alayhis-Salaam) alipewa herufi kumi na tano na Aadam (´alayhis-Salaam) alipewa herufi ishirini na tano. Yote hayo yamekusanywa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na watu wa Nyumbani kwake isipokuwa tu herufi moja ambalo Allaah amelificha Kwake Mwenyewe.

  • Mhusika: Ni´matullaah bin Muhammad al-Jazaairiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Anwaar an-Nu´maniyyah (01/34)
  • Imechapishwa: 07/12/2018


Takwimu
  • 287
  • 373
  • 1,819,055