Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab anawapa udhuru washirikina?

Swali: Je, imethibiti kuwa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema kuwa baadhi ya washirikina wanapewa udhuru kwa ujinga? Ni kipi kigezo cha kupewa udhuru kwa ujinga?

Jibu: Sijaona hili. Angalia maneno ya kijinga yanavyoenezwa! Wapewe udhuru kana kwamba hawakutumiwa Mtume wala hakukuteremshwa Qur-aan wala Sunnah? Yote haya hayajulikani leo? Ujinga umeisha – himdi zote ni za Allaah – kwa kutumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa kuteremka Qur-aan na Ahaadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ujinga utaendelea mpaka lini? Lau tutakadiria kuna mtu anayeishi mbali kabisa ambapo hafikiwi na Qur-aan wala hafikiwi na kitu na wala hasikii kitu, bali amebaki katika maumbile yake alozaliwa, huyu ndiye mwenye kupewa udhuru. Ama leo watu wote duniani wanasikia Qur-aan kwenye vyombo vya khabari na kwenginepo, hakukubaki udhuru juu ya ujinga. Pamoja na kwamba wale wenye kusema kuwa wana udhuru kwa ujinga wengi wao wamehifadhi Qur-aan na haishangazi ikawa ni kwa visomo vyake kumi, pamoja na yote haya anawaomba maiti na anawataka uokovu maiti! Ujinga uko wapi?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-9.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020