Hii ni talaka ya ki-Sunnah au Bid´ah?

Swali: Mtu akimwambia mke wake ndani ya twahara ambayo hakumwingilia “Ukitoka nyumbani basi nimekutaliki”. Akatoka katika twahara aliyomwingilia. Je, Talaka hii ni ya ki-Sunnah au ya ki-Bid´ah?

Jibu: Hukumu imefungamana na ule wakati wa kutokea jambo. Hii ni Talaka ya ki-Bid´ah kwa sura kama hii.

Lakini lau angelisema kumwambia “Ukitwaharika na halafu nikakwingilia nimekutaliki [ikiwa utatoka nyumbani]”, katika sura hii atakuwa ameifungamanisha na Talaka ya ki-Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-9.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020