Salafiyyah ndio Kundi la Allaah


Ama kuhusiana na kwamba anawaita Salafiyyuun kuwa ni “Talafiyyuun”[1], waharibifu, mimi nakubaliana na yeye pia. Ninasema kuwa Salafiyyuun ni Talafiyyuun, waharibifu, lakini wanaiharibu Bid´ah na wanaiponda wakati huo huo wanaihuisha Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Salafiyyuu ni rafiki bora na watu bora! Lakini Salafiyyuun si maanishi watu wa makundimakundi. Kwa neno “Salafiy” namaanisha mtu mwenye kufuata yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bila ya kuwa na chama. Mimi napinga vyama vyote, sawa bila kutazama rangi au majina. Ummah wa Kiislamu unatakiwa kuwa kundi moja.

وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ

“Atakayemfanya Allaah kuwa ni  rafiki na Mtume Wake na wale walioamini, basi [itambulike] hakika kundi la Allaah ndio washindi.” (05:56)

Kundi la Allaah ni wale waliyoshikamana barabara na Shari´ah ya Allaah (Ta´ala) kwa uinje na kwa undani na wanakataa Bid´ah kubwa na ndogo. Haliachi kauli ya yeyote itangulie Kauli ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kundi ambalo halitangulii mbele ya Allaah na kunyanyua sauti mbele ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haliachi kauli ya yeyote kutangulia mbele ya kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili ndio kundi la Allaah[2], Hizbullaah, ambao ni Salafiy na Athariy. Sisi wote ni wajibu kujiunga nalo na kutokomeza madhehebu ya makundi mengine yote ambayo kwa uhakika yako katika madhara ya Uislamu. Kwa kundi la Allaah, Hizbullaah, namaanisha tu yule ambaye yuko katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Walio kinyume nao, sio katika kundi la Allaah hata ikiwa watajiita kuwa ni kundi la Allaah.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/mwenye-kusema-salafiyyah-ni-manhaj-haribifu/

[2] Tazama http://firqatunnajia.com/salafiyyah-ni-kundi-la-allaah/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=c5y44OVTo3s&feature=emb_title
  • Imechapishwa: 06/09/2020