Swali: Kuna mtu alikuja kumposa dada yangu. Mtu huyo hahifadhi swalah na anavuta sigara. Baba yangu amekubaliana na jambo hilo isipokuwa tu mimi sikukubaliana naye. Ni zipi nasaha zako?

Jibu: Kipi kilichobaki ikiwa hachungi swalah? Usimamizi ni wa baba yako na hauko kwako. Ikiwa hachungi swalah basi nendeni mahakamani ambapo watamvua usimamizi baba na watauhamisha kwa aliye baa yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 25/02/2022