Swali: Nasumbuliwa na mzio puani. Ninapopandisha maji puani wakati wa kutawadha, basi hali ya mzio inakuwa mbaya zaidi. Kipi natakiwa kufanya wakati wa kutawadha?

Jibu: Mosi nenda kwa daktari akutibu:

“Allaah hakuteremsha maradhi yoyote isipokuwa aliteremsha pia dawa; ameijua yule mwenye kuijua na ameijahili yule mwenye kuijahili.”[1]

Pili ikiwa maji yanakuathiri basi usipandishe maji sana. Pandisha maji kidogo tu. Ikiwa huwezi kabisa kuingiz maji puani, basi fanya Tayammum. Tawadha na fanya Tayammum badala ya kuingiza maji puani.

[1] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” (3/75). Swahiyh kwa mujibu wa Ibn ´Abdil-Barr katika ”at-Tamhiyd” (5/283).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 25/02/2022