Pindi unapochenguka wudhuu´ wa imamu

Imamu akipatwa na hadathi basi anaweza kuchagua moja katika yafuatayo:

1 – Akiwa karibu na mahali pa kutawadha, basi awaashirie watu wabaki katika swalah yao kama walivyo kisha yeye atatawadha, atarudi na atajengea pale alipokomea.

2 – Lisipowezekana jambo hilo, atamuashiria mmoja nyuma yake ashike nafasi yake ili awakamishie swalah yao.

3 – Kila mmoja akamilishe swalah yake kivyake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 141
  • Imechapishwa: 02/07/2022