Pesa anazopewa mkimbizi anapofika nchi za makafiri

Swali 34: Wakati myemeni anapofika Marekani basi wanaomjua wanampa pesa kwa mnasaba wa kufika kwake. Je, azirudishe nazo ni katika haramu?

Jibu: Tayari tumeshajibu jibu swali hili. Uchaji zaidi ni yeye kutozipokea. Akiwa ni mwenye kuzihitajia basi dhambi ni kwa wale wenye kuyafanya moja kwa moja. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitaamiliana na mayahudi pamoja na kuwa anatambua kuwa wanakula ribaa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 72
  • Imechapishwa: 28/12/2019