569- Nlimsikia baba yangu Ahmad akiulizwa kuhusu bwana mmoja ambaye anaishi katika nyumba ambayo inatakiwa kutolewa zakaah. Akajibu: “Ndio.” Kukasemwa: “Ni nyumba kubwa.” Akajibu: “Nataraji hakuna neno.” Kukasemwa: “Anaye mfanya kazi pia.” Akajibu: “Nataraji hakuna neno.” Kukasemwa: “Anaye farasi pia.” Akajibu: “Nataraji hakuna neno kama anamtumia farasi kwa ajili ya kupambana katika njia ya Allaah.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 118
  • Imechapishwa: 19/02/2021